CEOInterviews.AI
Start App
William Ruto
President, Kenya

Live: Ruto Attends NYOTA Capital Disbursement, Buntwani Waterfront Park Malindi, Kilifi County

📅 Feb 05, 2026 Mutembei TV 139 MIN 1887 VIEWS 38 SEGMENTS · 16 SPEAKERS
TO SHARE YOUR STORY WHATSAPP US ON +447984970048 Mutembei TV is the leading channel in Kenya and Africa in general dealing in news around Kenya and outside the country.We do politics as well as local news.You will get the latest news as they happen.Our idea is to Educate, inform and entertain you guys.In case you want to contact us for any event that you want covered kindly send us an email [email protected] for subscribing and feel at home. SHARE AND SUBSCRIBE!! Follow us on: Website: https://mutembeitv.com/ Twitter :   / mutembeitv   FACEBOOK:   / mutembeitv   -----------------...

Questions asked in this interview

1
  1. 1:34:02Na am very happy katika hiyo program pesa ambayo tunatoa Marekani, pesa tunatoa Ulaya pesa tunatoa sehemu zingine za dunia hii imefikia kuongezeka kwa bilioni moja in two years. Nyi mnanielewa?
Unknown 0:00 ↗
Leo tunashukuru kwa kujumuika eneo hili. Tunashukuru kwa kukutana na rais wetu mpenzi kipenzi cha wananchi wake na taifa hili la Kenya. Ya Allah kwa kazi kubwa anazofanya na anazo kuzifanya tunamuombea umpee ujasiri nguvu ukakamavu na hekima zaidi ya kuongoza nchi yetu na kutusongesha mbele pamoja na mama yetu mama wa taifa amsimamie amuongoze na ampe imani katika kusimama na rais katika safari hii pamoja. Ya Allah tunashukuru kwa fursa hii tunawaombea viongozi wetu wa jimbo letu la Pwani na viongozi wetu wa taifa zima ya Allah waongoze wasimamie wape ujasiri na ukakamavu katika kazi zao na katika kutusimamia katika kuhudumia wananchi ya Allah walinde waongoze ya Allah vile vile tunashukuru kwa fursa hii sisi vijana kukutana hapa na kupata fursa hii ya maendeleo ya kufanya mipango ya kuendesha uchumi wetu kama vijana ya Allah tusimamie tuwezeshe na tuweze tukufikia ya Allah tunashukuru kwa projecti hii ya nyota ya Allah tusimamie iwe yenye kutuongoza kutusimamia kutushikanisha vijana na kutuendeleza katika kutekeleza uchumi wetu kuusongesha mbele ya Allah amin.
Tuamini na tuombe. Asante mtakatifu Mungu ishie na kutawala nakushukuru kwa ajili ya saa hii uliyotupa kuiona wakati na majira haya Bwana nakuinulia mheshimiwa rais na jamii yake mikononi mwako. Naomba ukawafunike kwa wingu lako la ulinzi wabariki Bwana na uwainue. Naomba uendelee kumuongoza rais wetu kwa hekima na maarifa yako katika njia ya amani na maendeleo. Wabariki na kuwaongoza hata viongozi wengine wote watakaoongoza taifa kwa njia inayokupendeza Mungu. Tena Bwana nakuinulia mradi huu wa nyota ulioteuliwa vijana kupitia rais wetu. Naomba Bwana uendelee kufanikisha mradi huu na ukawape vijana akili na maarifa ili mradi huu ukaweze kuwainua kimaendeleo na kimaisha. Bwana nakuinulia hafla hii ya leo mikononi mwako. Oneekana wewe katika kila jambo. Nafunga kila akili na mawazo ambayo yanaweza kujiinua kinyume na hafla hii katika jina la Yesu yashindwe tuongoze Bwana kuanzia mwanzo hadi mwisho ukitufanikisha vyema utukufu na heshima tutakurudishia wewe. Nimeomba nikijua umetenda kwa utukufu wa jina lako. Amen.
Amen. Naomba tuweze kuketi. Mheshimiwa Rais Daktari William Samuel Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya na amri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi Profesa Abraham Kithure Kindiki. Naibu wa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Speaker of the Senate, Mheshimiwa Amazon Kingi, mheshimiwa Wickley Foparanya waziri wa ushirika, mheshimiwa Salim Vuria waziri wa michezo na maswala ya vijana mawaziri wote waliofika mahali hapa. Makatibu wote wakiongozwa na PS wa biashara ndogo ndogo Madam Suzan Mangeni, gavana wa Kilifi mheshimiwa Gideon M'aro, magavana wote ambao pia wamefika mahali hapa wabunge wakiwemo wabunge wa serikali gatuzi, Chimya yao Fan ambaye anawakilisha World Bank. Ah viongozi wote wa serikali kuu na serikali gatuzi wafanyibiashara vijana wa kutoka Kilifi, Tana Riva na Kilifi, Tanaiva na Lamu wakiwa mahali hapa. Mheshimiwa rais niruhusu kwa nafasi hii nimkaribishe PS Suzan Mang'eni ambaye atatuongoza katika ratiba yetu ya siku ya leo. Tumkaribishe kwa makofi tafadhali. Na nikiwakumbusha wale ambao wote watapata nafasi ya kuongea tuongee kwa ufupi ili tumpatie rais nafasi ya kuongelesha vijana. Karibu madam PS.
Suzan Mangeni 4:06 ↗
Asante mheshimiwa rais William Ruto. Makamu wa rais Profesa Abraham Kithure Kindiki, mawaziri, viongozi wote ambao mko hapa mheshimiwa rais niruhusu I stand on the protocols as I've been observed by Mike Gitonga. Leo hivi tuko hapa katika hii cluster ya Kilifi ambayo inajumuisha kaunti tatu Kilifi, Lamu na Tana River. We have a total of over 5,000 beneficiaries ambao leo wako tayari kuanza safari yao maalum ya kufanya biashara. Tungependa kwanza kukushukuru kwa kutenga nafasi na kuja kujumuika na sisi na hawa vijana wetu. Maanake tunajua kuwepo kwako hapa kutawapatia maarifa moja ama mbili jinsi watakavyoendesha biashara zao. Kwa hivyo yangu kwanza ni kuwajulisheni hawa vijana ambao walijikakamua wakachukua simu yao wakaamua simu yao ni ya kuwasongesha mbele kimaisha na wakaapply. Ilikuwa safari mrefu sana from last year in March wamengoja wakangoja hadi siku ya leo hayawi hayawi wamefanya nini asanteni. Kwa hivyo leo hapa tuko na vijana kutoka Tana Riva. Tana Riva hoye. Eh ni kama hamjaonekana Tanaariva. Hoye hoye. Tuko na vijana kutoka Lamu. Lamu mambo poa. Hebu nione mikono ya Lamu Lamu. Lamu lamu lamu. Asanteni sana. Naona kama nimemaliza nimesahau. Haya watu wa Kilifi mamboa. Hebu nione mikono ya Kilifi. Kilifi. Kilifi Kilifi Kilifi. Kilifi kilifi. Na mbona nyinyi ni wengi? Mmekuja mbili mbili mko home mmejipanga. Haya mheshimiwa rais niruhusu niintroduce kwanza makatibu ambao tunafanya nao kazi katika ile Hall of Government Approach wasimame tu mahali wapo msimame makatibu wote nikitaja jina tuko na katibu Dr. Raymond Omolo ambaye amesimamia interior. Tuko na katibu Patrick Kilemi ambaye amesimamia cooperative. Tuko na katibu kutoka kijana wa nyumbani kutoka Lamu ambaye amesimamia mbona mbona sijawaambia ni nani? Mnapiga makofi nyinyi si wazuri anaitwa nani? Anaitwa nani? Okay. Amesimamia investment. Tuko na katibu Aden Miller ambaye amesimamia mambo ya shipping na maritime. Tuko na katibu Idris Dokota atoka Tana River. Tuko na msemaji wa serikali aitwa nani? Aisha no Mwanaisha. Eh mwanaisha Chizuga. samahani tuko na katibu ambaye amesimamia mambo ya science na research huko huko innovation hivo hivo anaitwa Profesa Shukut tumpigie makofi haya watu wa Kilifi cluster mambo sasa mheshimiwa rais hawa unajua wanatuita sisi watu mimi ni mtu wa bara lakini wameniruhusu kidogo nifanye kitu tu kile ndio tuone kama wako ready testing na mambo yao sindio najua sijaintroduce katibu mwingine hapo nataka akuje top sher top sher njoo njoo top sher njoo njoo sasa kabla top shot hajaongea nataka nyinyi wote msimame mkaribishe kama mmekaribisha mheshimiwa rais na mmetufurahia na mko Uko tayari simameni kila mtu asimame kila mtu asimame we DJ wacha kuleta machanganyiko kidogo kila mtu asimame na nyinyi mnajua hii pesa inakuja kwa njia ya kwa njia ya nini tunataka kuhakikisha nyota sindio are you ready haya tuhakikishe nyota zetu na tushike simu zetu juu ndio sasa upepo vizuri sindio na usimbo DJ wacha machanganyiko nyumbani DJ sikiza maneno wacha machanganyiko fanya hiyo wacha machanganyiko haya haya haya haya haya machanganyiko nataka lero lero ni lero lero lero ni lero Haya haya haya haya haya mheshimiwa rais utatusaidia hapa kidogo.
Fikirini Jacobs 11:23 ↗
Asante sana vijana power power hapana vijana poa poa kwani nyinyi Mnaishiwa pawa mchana bwana vijana poa poa. Asante sana mimi naitwa Fikirini Jacobs ni kijana na ni katibu wa vijana katika wizara ya vijana na michezo kwenye administration ya mheshimiwa rais Dr. William Ruto. Mimi nimekuja hapa kwanza kuambatana na mheshimiwa rais kushuhudia vijana wetu zaidi ya 4000 leo hii kutoka Lamu, Tanaiva na Kilifi wakianza safari ya kuwa wanabiashara katika hili taifa la Kenya. Na your excellency mimi nataka nisimame kwanza nitoe shukrani zangu nyingi sana za dhati kama kijana wa taifa la Kenya. Your excellence miaka 26 ndani ya karne ya 21 taswira na malengo ya kijana wa taifa la Kenya yamebadilika excellency ni nani katika historia ya taifa hili angefikiria kwamba kijana kutoka Basuba ndani ya bony forest kijana kutoka Shangia huko kupita Marekani kijana kutoka Bandara Salama Dindiri Bombi Oda Wakanda huko Tana Riva angefika hapa leo your excellency bila kujuana na mtu yeyote bila kujuana na chief bila kujuana na kiongozi bila kujuana na deep state bila kujuana na system yaani your excellency deep state na system ya vijana wa taifa la Kenya ni simu yao na uwepo wa nyota kupitia baraka zako excellence vijana hawa walishika simu wakaweka star 254 hash wakaweka imani wakafuata maagizo wakaenda training na leo hii wamefika hapa asubuhi sana excellency wewe uwapange na mimi nikimalizia nataka niwaambie vijana wetu mheshimiwa rais ametupanga ametimiza jukumu lake na mheshimiwa rais nimemsikia kwa sababu leo hii tukimaliza itakuwa kaunti ya 41 ambao watawari wamepata pesa zao za nyota na nimemsikia mheshimiwa rais amesema mara nyingi hii pesa ya nyota hata fuliza hata hla fund pia haigusi yaani unaipata kikamilifu lakini mimi nataka nimalize sasa hiyo excellence mimi nilikuwa nafikiria kwa kuwa wewe umering fence hii pesa isiguswa na hasla fund isiguswa na fuliza pia mimi nimeomba ruhusa kwa bishop katite hata fungu la 10 pia iring fence your excellence isiguse asante.
Owen Baya 14:05 ↗
Makofi kwa fikirini jacob. Haya niko tu na mambo mawili ya kwanza tutakapotoka hapa tunaenda kufanya mentorship tunaelewana mentorship ya two months kwa hiyo mentorship tunataka kuona unapoanza biashara yako unaanza biashara gani kwa sababu sumam plan all sindio ready to go wale ambao mko na biashara ambazo zinaendelea existing business mlifunzwa vizuri na mkaambiwa jinsi mnavyoweza sasa kupangapanga biashara yenu kuexpand ama labda tena mfanye biashara ingine kando na ile ambayo mlikuwa mnafanya sindio hiv kwa hivyo tutaenda mentorship period ya 2 months tuko na wale wataalamu wetu ambao walikuwa wanawatrain those trainers and mentors are going still to be with you for that period of two months after that we will come back to classroom training. mnakumbuka mahali tulikuwa tunatrainiwa this time round for 3 days and not four days na itakuwa training maalum ile ambayo sasa inaweza kuklink up sasa kwa soko kama wale ambao mnafikiria utapataje soko la kuuza bidhaa zako watakuwa wanawafanyia linkages kama wale ambao mnataka pesa kiasi kingine ya ku you know additional funding for your business again mtaweza kupata hapo ushauri mtaweza kupata kupata pale mwelekezo jinsi mnaweza kutop pesa ya kufanya biashara zenu immediately after that 3 days mtapewa tena ile pesa yenu sasa ile iliyobakia tunaelewana ikifika hapo mnapiga makofi mtapewa mtapewa pesa yenyu itakayo imebakia kwa hivyo ni discipline yenyu ambayo itafanya so the second disbassment.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Dr. William Samoi Ruto naibu wake Profesa Kithure Kindiki fireman na ndugu viongozi wote ambao wako hapa akiwa gavana wetu wa Kilifi. Vijana hoye vijana hoye hoye. Harujasikia hiyo sauti? Vijana hoye hoye. Basi mimi kama mmesikia mimi ni naitwa Owen Baya. Mimi ni mbunge wa Kilifi North lakini pia nahudumu kama deputy majority leader wa National Assembly. nachukua hii fursa mwanzo kuwakaribisha hapa Kilifi county na nichukue ile kazi nimepewa kidogo ya kukaribisha wabunge wenzangu niwaulize wakae hapa mbele ili tufanye haraka haraka tafadhali sitting MPs ambao wako tupande hapa juu ya jukwaa ili niwaintroduce lakini niseme rais tunakushukuru sana kwamba vijana wa Kenya sasa wanatambulika leo tumegadha hapa kwa sababu sababu ya maneno ya nyota karibuni sana viongozi kunie na maana nisicha nafasi barabarani kuendeza nikose na kukwa mchini yaani nikukopi sana maherema kila magura ati mwenye kumboke gama ambaye kajura sitting mping mp karibuni sana mnaona timu ya pwani sindio mnawaona eh hawa ndio wawakilishi wetu wa pwani. Eh haya basi sasa huyu bwana anaitwa Ken Chonga. Ken kitonga mbunge wa Kilifi South Chairman Labor Committee National Assembly. Tusalimie. Sawa. Asante sana. Next. Huyu bwana anaitwa Stanley Muthama. Huyu ni mbunge wa Lamu. Eh hawa walamu wako noma wako rada. Huyu ni Kten Ruida mbunge mama kaunti wa Lamu. Ehe huyu anaitwa Machele mbunge wa kule Mombasa Mvita. Thank you. Thank you machele. Huyu ni mama kaunti wa Mombasa mama Zamzam. Asante sana. Na huyu anaitwa PK mpaka kieleweke. Paul kataa na mbunge wa Kaloleni. Ah ah wewe vipi mbona hupigiwi makofi? Sawa. Asante sana. Huyu ndugu yangu anaitwa bwana Chome ni mbunge wa kule Taita Voi. Asante sana. Na huyu mrembo mnamuona? Mnamuona huyu anaitwa Mudhoni Marubu mbunge wa mama kaunti wa Lamu. Thank you. Thank you. Thank you. Na huyu ni Canon Shake mbunge wa Mwatate kule Taita Taveta. Wo haariva wako rada. Morada huyu anaitwa nani ati? Anaitwa kumbe ana jina ingine. Ah huyu mbunge wa kule Bura. Asante sana huyu mwanzo unataka akae kando huyu? Huyu akae kando. Wacheni huyu akae kando mwanzo. Mnamjua huyu? Huyu anaitwa Mishi Mboko mbunge wa Likoni. Asante sana. Thank you sana. Na huyu mnamjua anaitwa anaitwa Kenneth Charo Tungule mbunge wa Ganze. Thank you. Thank you. Na huyu mrembo anaitwa Masito. Anaitwa nani? Masito. Anatoka kule Kwale ni women rep wa Kwale. Apewe. Apewe. Ehe. Apewe asipewe. Apewe. Apewe asipewe. Apewe. Lakini apewe nini? Hakuna. apewe mbunge wa rabai. Asante sana na huyu sijui ni kitinda mimba ama ni mwana wa kwanza. Huyu amerudi bunge juzi. Huyo ni mzee wetu Hari Kombe mbunge wa hapa magharini. Asante sana. Na huyu ni kiongozi chairman wa departmental committee ya trade pale ndani ya bunge ya kitaifa. Ni mgeni wetu maalum kutoka kule western anaitwa Bernard Shinali. anapanga hii. Yeye ndiye anapanga hii pale bunge. Asante sana. Wacha nimalize huyu anaitwa Kituku. Kituku. Kituku. Kituku. Watu wa alamu mnamjua huyu? Eh. Anaitwa Kituku. Huyu Kituku ni mbunge ni senet wa Lamu. Sawa. Asante. Sasa ile nimebakisha hawa wazee nataka waongee dakika moja moja na mimi nitakuwa hapa nitakuwa na kibonyezo. Mwanzo nilete huyu mrembo mnamuona huyu? Eh kwani kuna akaunti iko na mbunge mrembo kama huyu? Hakuna. Kuna akaunti hapa iko na mbunge mrembo kama wakilivi anaitwa Amina Myazi. Huyu ndiye mbunge host wetu wa hapa Malindi. Karibu sana Amina.
Amina Myazi 25:14 ↗
Asante sana deputy majority leader mheshimiwa rais mheshimiwa deputy president spika mawaziri ambao wako hapa PS wabunge na viongozi nyote hamjambo? Hamjambo tena mimi leo niko na furaha na nataka nichukue fursa hii niwakaribishe hapa Malindi kama mlivyosikia mimi ndio ni mbunge wa hapa kwa hivyo mjue kwamba hapa Amina yuko home kwa hivyo nataka niwakaribishe feel free Malindi ni mji wa watalii na nyinyi nyote mmeweza kufika hapa tumeona leo biashara mheshimiwa rais zimeng'ara tangu jana hoteli zilikuwa zimejaa hapa Malindi so sisi kama watu wa Malindi we really appreciate that and we don't take that for granted la pili ni kusema ya kwamba vijana nyinyi ni watu muhimu sana si mnaona huo umuhimu wenu leo hii nyinyi vijana mmeweza kuleta rais wa nchi yuko hapa yuko hapa na nyinyi ama hayuko hapa? Deputy president yuko hapa ama hayuko hapa? Mawaziri wako hapa ama hawako hapa? PSS wako hapa? Hawako hapa? Viongozi wengi wameweza kufika hapa ili kuja kusikia sauti yenu nyinyi vijana ili tuweze kujua tutashirikiana vipi na tunaenda vipi kule mbele. Kwa hivyo na nyinyi pia mjipigie makofi. La tatu mheshimiwa rais sisi tulikuwa tunaona unazunguka kule kutuanisha hizi pesa za nyota tukasema na huku kwetu Pwani utafika lini? Amefika ama hajafika na leo watu wa Pwani sisi watu wa Kilifi Tana Riva na Lamu pesa zitaingia ama hazitaingia? Si mambo yatakuwa ni mazuri leo ila zile pesa zikitoka vijana wangu niseme nisemea pesa zikitoka isiwe ni sababu ya wewe kukosa heshima pale nje. Mnajua rais ni mtu ambaye anampenda Mungu sana ni mcha Mungu na anajua ile pesa ikitoka ni ya wewe kwenda kufanya nini? Kwenda kujisaidia kwenda kufanya biashara kwa hivyo chukua hiyo pesa with a lot of seriousness. Hakuna rais mwenye ambaye ameshawahi kuleta program kama hii ambayo inaweza kuempower vijana. Ama nyinyi mnajua rais mwingine ambaye anaweza kufanya hivyo? Mnamjua mwingine ambaye anaweza kufanya hivyo? Afadhali ile sahani yenye ambayo uko nayo pale mezani unaiona na chakula kuliko kuondoka pale kwenda kwengine kutapatapa. Sisi tutashiba hapa kwa William Samoi. Asante sana na Mungu awabariki.
Owen Baya 27:46 ↗
Asante sana Amina. Sasa nimuite women repu wetu wa Kilifi mama G mama Mbeyo.
Mama Mbeyo 27:53 ↗
Asante mheshimiwa Owen. Vijana na nyota hoye hoye sijasikia. Wakilifi hoye hoye watana hoye walamu hoye naitwa mama g mama lao mheshimiwa mbeyu mwanjanje mheshimiwa rais makamu wa rais mawaziri magavana wote ps viongozi wote wabunge mc na machifu wetu leo ni siku ya furaha si ya furaha vijana mna raha hamna raha raha Yaani hii pesa inaingia kwa simu yako ishawahi ingia kweli hii Kenya tangu uzaliwe. Si tumpigie makofi rais wetu Dr. William Samuel Ruto mshawahi kuona nyingine kama hii? Ah ah tangu uzaliwe ushaona mpango kama huu rais wetu aendelee asiendelee? Eendelee. Nataka kusikia hilo moja. Rais aendelee asiendelee? Kenya kuna mwingine kama daktari. Hakuna. Ushawahi kuona mwingine kama daktari? Hakuna. Samuel Ruto ushawahi kumuona? Wengine ni simba wa kuchonga hawatishi lolote hapa. Furaha yetu vijana mmeanzishiwa huu mradi. Kuweni makini. Miseme siseme. Umeambiwa hizi pesa hazilipi fuliza hazilipi hata. Sindio? Hii pesa isinunue mogokaa ndani ya pwani kwa vijana wetu. Upo niseme niseme ifanye biashara isinunue nini isinunue nini hatari za mogoka niseme nisisemea hatari za mogoka rais asikie asisikinunue nini hatari za mogoka niseme nisiseme sema hatari za mogoka rais asikie asisikie zinaharibu hawa vijana mheshimiwa rais hatutaki hii pesa iwe diverted watumie kwa biashara wajiinue. La mwisho kama wewe ni kijana uko hapa hujachukua kura, hujajiandikisha kura, ukitoka hapa kajiandikishe kura. Silaha yako ya kuendeleza nyota ndani ya Kenya. Kweli uongo? Silaha yako ya kujiendeleza kuanzia 2027 mpaka 2032. Ukweli uongo. Kama huna kura utaweza kuja tena hapa. Rais Samuel Ruto aendelee asiendelee aendelee. Mungu awabariki tuwe pamoja. 2027 tuko na rais mpaka huko mwisho huko Mungu aseme. Asanteni sana. Thank you so much.
Owen Baya 30:32 ↗
Haya asante sana mama J. Sasa nimuite mzee wetu huyu lakini mwenyewe hapendi kuitwa mzee bado ni kijana sindio senetor wetu wa Kilifi Mkoi Steward Mazayo karibu sana mkoi.
Stewart Mazayo 30:44 ↗
Asante sana ndugu yangu Owen. Mheshimiwa rais daktari Sam Arap Ruto na kigugumizi kidogo tafadhali. Eh ah naibu wa rais Profesa Kindiki mawaziri wetu ambao wamewahi kufika hivi leo ndugu zangu ah waheshimiwa gavana wetu wa Kilifi kaunti itifaki zote zikizingatiwa nataka niseme kitu kimoja tu ya kwamba sisi Sisi watu wa Pwani ama sisi watu wa upande huu wa kutoka Kilifi, Tana Riva na Lamu. Vijana wetu tuko na bahati sana. Bahati sana kwa sababu mradi kama huu tokea Kenya ipate uhuru hakuja kuwa na mradi kama huu wa kusaidia vijana kujiweza kujinisha kuweza kujiinua katika biashara. Na mradi kama huu kama umepatikana ni lazima tuone ya kwamba tumeutumia vilivyo ili kujiendelesha maisha yenu. M nataka kutoa kongole sana kwa mheshimiwa rais kufanya juhudi zake zote anazoweza kuona ya kwamba mradi kama huu umekuja hapa kwetu ndani ya Kilifi, Tana Riva na Labo. na utaendelea kuwacover Kenya yote hii. Kwa hiyo mimi kama nataka kuwaambia uhusia I want to advise you pesa uitumie kwa manufaa ya kuweza kujifaa wewe mwenyewe leo na kesho na kesho kutwa. Na ukitumia vizuri tumeambiwa itaongezwa ingine ili uweze kuendelea katika maisha yako. Hii pesa hii si ya kwenda kulipa mahari. Najua nyinyi ni vijana wengi wenu hamjaoa. Kwa hiyo si pesa ya kutumia katika zile njia zingine ambazo utajiharibia wewe mwenyewe. My advice is take care of this money, use it properly ili iweze kukuinua wewe na jamii yako. Mheshimiwa Rais nataka niseme asante sana kwa kuweza kuleta huu mradi kwa kuweza kusaidia vijana wetu wa kutoka Tana Riva, kutoka Lamu na hapa kwetu Kilifi. Asanteni sana.
Owen Baya 33:35 ↗
Asante sana Mkoi. Basi nichukue hii fursa niulize MCA wako hapa wakilifi. Tafadhali wasimame MCA wa Kilifi county. Kilifi. Kilifi MCA. Tuwapungie mkono hawa MCA wetu wa Kilifi. Asanteni sana kwa kuja. Thank you very much. Niulize basi MCS wa Lamu kama wako hapa. Lamu Lamu wale MCAs wa Lamu. Do we have MCAs from Lamu? We don't have MCAs kutoka Tana Rivera ambao wako hapa. Tana Rivera MCA ambao wako hapa. Basi nichukue nafasi hii wale chairman wa boards national parastatles kama wako hapa chairpersons chairman wa boards wa wote wale haya asanteni sana directors na wote wale wako hapa basi mheshimiwa rais mimi niseme hivi if i was a young man during your presidency wakati huu na umenipatia 50,000 shillings ya kufanya biashara in the biggest farmer than you would be a bigger businessman than you because I would invest the money and take care of it, ring fence it and make a better business person. Umenielewa vile nimesema? If I was a young person sitting there today, nimepewa 50,000 leo, I would become a very big businessman over 3 years period. Ni pesa ngapi? Ni 20 ama ni 50? Eh hiyo hata hiyo 20. Naongeza mwaka mmoja instead of three, I would make it four years and I would become a bigger businessman. kama uko na akili utatumia hiyo maneno. Asanteni sana. Mimi basi nichukue nafasi hii kwa heshima kubwa mheshimiwa rais nimwite waziri wa MSM Waziri Oparanya. Karibu sana. Tupigie makofi. Huyu waziri ndiye anafanya hii pesa inakuja hapa. Karibu karibu karibu.
Wycliffe Oparanya 35:34 ↗
Mheshimiwa rais mheshimiwa naibu wa rais wendangu mawaziri PSS na wananchi wote hamjambo? Hamjambo. Basi nitachukua nafasi hii kwa ufupi kabisa. Nataka niseme hivi, tumekuja hapa mambo ya biashara. Kwa biashara wanasema time is money. Time is nitawaita watu wa churchi hapa. Nikiwaita hapa please one minute. Na ukija hapa tuko kwa mambo ya biashara. Tunataka tusikize mambo ya biashara kama wewe unajua biashara. So i call few people just to come and create and if they have anything to say it must be restricted to what we are here for. Nataka nimuite director wa bank let me call the director of World Bank Kimao Fan.
Chimya Fan 36:55 ↗
Thank you thank you very much CS your excellency mr president your excellency vice president CSS governors and members of parliament the talented use of kenya kapariza asubuhi Good morning to you all. I'm very honored to join you all here on the regional rowout of Niota in this beautiful city. Some of you may ask why Neota and why is Neota important? My answer is very simple, your excellency, is because Niota is a innovative, inclusive and transparent initiative at scale to address what I believe is the biggest development challenge Kenya faces today and that is jobs and that's why we at the World Bank wanted to support you. Indeed, your excellency friends, the World Bank does only three things in Kenya and that is jobs, jobs and jobs. In addition to patterning and supporting you in implementing Neota, our entire program is squarely focused on supporting Kenya to create more better and more inclusive jobs from supporting your policy reforms to make doing business easier to investing in energy roads, digital technology and to skills and to specific sectors like agriculture. The sole objective is to support Kenya to create more and better jobs and we continue to do so. Thank you Mr. President for your leadership and support for the Neota program. But ultimately ladies and gentlemen friends the success of Niota will be measured by how much employable that the beneficiaries will become and how many of you will be able to create businesses not just employing yourself but employ millions others and will be measured by ultimately how many decent jobs that we can help to create in this great country and we at the World Bank will continue to support you in this journey. Asante sana.
Wycliffe Oparanya 40:02 ↗
Thank you. Let me acknowledge my colleagues who are here. You will have a chance to come here and speak. We have CS Alice Wahome. You not come to speak just to car your hands. You be given a chance of housing. Affordable housing. Si mnasikia mambo ya affordable housing. Ndio huyo Alfred Mtua Kazu ndio huyo. Salim Mvuria mambo ya vijana ndio huyu Hassan Joho. Mambo ya mining na ile mambo ya fishing. Basi nitachukua nafasi hii niwakaribishe magavana ambao wako hapa. Salamu tu. Nikianza na gavana wa Lamu. Gavana wa Lamu. Maharage yako jikoni nimeshayapika. Nangojea sukari ya Bwana haijafika. Lambwa lambwa. Haya vijana hoye hoye vijana hoye hoye.
Gavana wa Lamu 41:25 ↗
Mheshimiwa rais mheshimiwa makamu wa rais spika wa senate magavanaor mawaziri wabunge mapura kubwa kuwa hapa na kwa niaba haswa wa vijana wa lamu tumefurahikia huu mpango wa nyota na niseme tu kwa vijana wa lamu kuwa kama serikali ya Lamu mkifanya biashara kwa huu muda mimi ni gavana hamtalipa liseni itakuwa ni bure na pia nitafungua afisi na nitaweka mfanyikazi pale awe anacoordinate na nyinyi mkiwa na maswali mkiwa mnahitajia usaidizi muweze kupata usaidizi kwa haraka kwa hayo mengi nasema Ema asanteni sana na vijana hii pesa ni ufunguo wa kuboresha maisha yenu kwa hivyo mzitumie vizuri vile inavyotakikana na nimshukuru rais na serikali yake na World Bank kwa kusimamia mpango huu na kuempower mayuth mbele iko sawa asanteni sana na Mungu atubariki.

15 more exchanges in this transcript

Sign in free to read the rest of this interview. No card required.

Sign in to read the full transcript

Cite this transcript

APA, MLA, BibTeX
APA

Ruto, W. (2026, February 5). Live: Ruto Attends NYOTA Capital Disbursement, Buntwani Waterfront Park Malindi, Kilifi County [Interview transcript]. Mutembei TV. CEOInterviews.AI. https://ceointerviews.ai/interview/686344/

MLA

William Ruto. "Live: Ruto Attends NYOTA Capital Disbursement, Buntwani Waterfront Park Malindi, Kilifi County." Mutembei TV, 5 Feb. 2026. Transcript, CEOInterviews.AI, https://ceointerviews.ai/interview/686344/.

BibTeX
@misc{ruto2026_686344,
  author       = {William Ruto},
  title        = {Live: Ruto Attends NYOTA Capital Disbursement,  Buntwani Waterfront Park Malindi, Kilifi County},
  howpublished = {Interview transcript, Mutembei TV. CEOInterviews.AI},
  year         = {2026},
  month        = {feb},
  url          = {https://ceointerviews.ai/interview/686344/},
  note         = {Speaker-attributed transcript with timestamps}
}